Huenda ukatatizika wakati wa kujisajili au kupokea taarifa kutoka kwa mwanatimu wa mauzo. Tafadhali angalia tena kwani upatikanaji wa bidhaa unaweza kubadilika.
Endeleza timu yako na ufurahishe wateja wako
Popote wafanyakazi wako wanapofanya kazi, tunawarahisishia mchakato wa kuitisha usafiri, kuagiza chakula na kupata huduma kwa wateja.
Jinsi kampuni maarufu zinavyotumia mfumo wetu
Rahisisha safari za kikazi
Iwe wanaelekea kwenye uwanja wa ndege au kwenye mkutano wa wateja mjini, wafanyakazi wako wanaweza kuomba safari katika zaidi ya nchi 70.
Wape wafanyakazi marupurupu ya chakula
Ongeza motisha na tija kwa kuruhusu timu yako iagize kwenye migahawa ya karibu. Ni rahisi kutoa ruhusa za bajeti na wakati.
Boresha manufaa ya usafiri
Anzisha mpango wako wa usafiri ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wako salama na wana motisha. Inafanya kazi kwa safari za asubuhi, saa za mwisho na usiku wa manane.
Safirisha hati kwa urahisi
Agiza unapohitaji, wewe na wateja wako mletewe mikataba mahali mlipo kupitia Uber. Ni rahisi na haraka kama vile kuomba usafiri.
Wafurahishe wateja wako
Toa shukrani zako kwa wateja wako kwa kuwapa Vocha wanazoweza kutumia ili kupelekewa chakula kitamu.
Watuze wafanyakazi bora
Tambua wafanyakazi waliofanya kazi nzuri kwa kuwapa kadi za zawadi ambazo wanaweza kutumia kulipia safari na vyakula katika miji kote ulimwenguni.
“Kwa kuzingatia muda ambao baadhi ya wafanyakazi wetu hutumia barabarani, mfumo wa Uber for Business huokoa muda mwingi.”
Mattie Yallaly , Msimamizi wa Usafiri na Gharama, Perficient
Vipengele vya hali ya juu ili kuokoa muda na pesa
Tumia utaratibu wa kiotomatiki kulipia gharama
Tunaungana na watoa huduma maarufu wa kulipia gharama kama vile SAP Concur ili kuchakata gharama za matumizi kiotomatiki. Wafanyakazi hawahitaji tena kufuatilia stakabadhi.
Badilisha mipango ikufae
Weka viwango vya safari na chakula kulingana na siku, wakati, mahali na bajeti. Pia unaweza kurekebisha mipangilio ya wafanyakazi mbalimbali, kama vile kwa kuwapa watendaji ruhusa ya kupata chaguo za safari za starehe.
Pata vidokezi vya kina
Ripoti za kila mwezi zinakupa uwezo mkubwa wa kuchanganua gharama na matumizi ya wafanyakazi wako, ili uweze kuboresha sera ya safari na chakula na kukuza faida zako.
Sababu ya timu zenye shughuli nyingi kupenda Uber for Business
Tenganisha shughuli za kikazi na za kibinafsi
Ni rahisi kwa wafanyakazi kutenganisha gharama za kazini na za kibinafsi kwa kubadilisha wasifu wao wa kazini katika App za Uber na Uber Eats.
Tumia App ile ile kote ulimwenguni
Programu hii inapatikana katika zaidi ya nchi 70 na miji 10,000, hivyo kufanya iwe rahisi kuomba safari na kuagiza milo kote ulimwenguni.
Wasiliana na huduma kwa wateja
Tuko hapa kwa ajili yako na wafanyakazi wako kila wakati. Kwa hivyo, ikiwa una maswali yoyote au unahitaji usaidizi wa kutatua tatizo, wasiliana nasi.
Biashara yako inazidi kuimarika. Tuko hapa ili kukusaidia.
Muhtasari
Kutuhusu
Huduma
Huduma
Kulingana na matumizi
Kulingana na tasnia
Usaidizi kwa wateja
Usaidizi
Nyenzo
Pata maelezo